Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwatunuku Kamisheni maofisa wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Chuo cha Mafunzo wa Kijeshi (Tanzania Millitary Academy ‘TMA’) kilichopo Monduli mkoani Arusha.

Rais, anatarajiwa kuwasili Arusha Novemba 22, 2021 ikiwa ni sehemu ya ziara yake pia atazindua hoteli ya nyota tano Grand Melia iliyopo jijini hapo.

Hata hivyo rais Samia anatarajiwa kufungua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama Novemba 23, 2021 ambapo maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapoitakuwa mwisho wa ziara yake.

Akizungumzia ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema ni neema Rais kufanya ziara mkoani humo mara mbili na kwamba jitihada zake zinaendelea kuzaa matunda hasa katika sekta ya utalii.

Aidha, amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais Samia wakati akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na pia kushiriki kwa wingi kwenye maadhimisho hayo kwani elimu itayotolewa inawahusu sana.

Maadhimisho hayo kwa mwaka 2021 yamebeba kaulimbiu isemayo “Jali Maisha Yako na ya Wengine Barabarani.”

Shirikisho la Wakuu wa Polisi (EAPCCO) kukutana Mkoani Kilimanjaro
Wasira awataka vijana kuwa wazalendo