Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa – JKT, Julai 10, 2023 yatakayo fanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Julai 8, 2023 Jijini Dodoma na kuwataka Wananchi kujitokeza kwa Wingi kushuhudia ukakamavu wa Jeshi lao, pamoja na kumsikiliza Rais Samia.

Amesema, “katika maadhimisho haya kutakuwa na matukio mbalimbali pamoja na ugeni kutoka ndani na nje ya Tanzania, wageni kutoka Balozi mbalimbali kama Israel pamoja na balozi nyingine.”

Aidha, Waziri Bashungwa amesema  kupitia Balozi ya Israel, kutakuwa na chanel ya kidiplomasia ambapo wanatarajia kuonesha picha za matukio mbalimbali.

Lipeni michango ya Wafanyakazi kwa wakati - Katambi
Moise Caicedo apanda thamani England