Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kitaifa Julai 25, 2023 ambapo, zitakafanyika eneo jipya ulipojengwa Mnara wa Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ambapo amewakaribisha wananchi wote mkoani huo na mikoa ya jirani ya Singida, Iringa, Manyara na Morogoro katika siku ya maadhimisho hayo.

Amesema, kabla ya kilele cha maadhimisho hayo kutakuwa na uwashaji wa Mwenge wa Mashujaa na kwamba yanafanyika kwa ajili ya kuwakumbuka mashujaa waliotetea, kupigania na waliopoteza uhai kwa ajili ya kupigania na kulinda uhuru wa nchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, amewaomba wananchi kutumia maadhimisho hayo kudumisha na kuimarisha umoja wa kitaifa, amani na utulivu, ili kutumia muda mwingi katika kubuni na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.

Hasheem Ibwe: Azam FC itashangaza 2023/24
Serikali yatangaza kusitisha malipo ya Walimu