Rais wa Jamhuri ya muungano waTanzania Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari yatayofanyika kitaifa mkoani arusha mei 3 mwaka huu.
maadhimisho hayo yatahudhuriwa na nchi sita za Afrika Mashariki zikiwemo Rwanda ,Sudani ya Kusini , Ethiopia, Kenya, uganda na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo(DRC).
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Jukwaa la wahariri Tanzania(tef) Neville Meena wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu siku ya uhuru wa vyombo vya habari .
Meena amesema maadhimisho hayo yatafanyika kitaifa na pia katika ngazi ya mikoa, aidha amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika siku tatu ambayo yatakuwa na mada ku wa tatu zitakazo jadiliwa ambazo ni uhuru wa habari na kisheria, mazingira ya kihabari, vitisho vinavyotolewa kati,a vyombo vya habari na maswala ya kidijitalikwenye vyombo vya habari.
”Maadhimisho hayo yatahudhuriwa na wadau wa haabri 400 kutoka ndani na nje ya nchi lengo ni kujadili changamoto za habari” amesema Meena
Amesema kuwepo kwa Rais Samia katika maadhimisho hayo ni fursa pekee ya kueleza changamoto zilizopo ndani ya vyombo vya habari
Naye Ofisa Habari Kitengo cha Habri umoja wa mataifa (UN) Stella Vuzo amesema katika kuadhmisha siku ya uhuru wa haabri wameona jinsi gani vyombo vya habari vilivyo msaidia mwananmke kusimama mwenyewe.
Stella amesema vyombo vya habari vimemfanya mwanamke ajiamini na kufanya maamuzi yake mwenyeweambayo yanaleta tija.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema ”Uandishi wa Habari na Chanagamoto za Kidigiti”