Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ataendelea kuwateua wanawake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi kwasababu asipofanya yeye hakuna atakayefanya kwa kiwango .
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Septemba 15, 2021 wakati akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Demokrasia duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

