Rais Samia Suluhu Hassan amesema hana tabia ya kutukuzwa wala kulinganishwa na Mungu na kwamba atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu wa kusikiliza maoni ya wengine.

Rais Samia Amesema hayo Rais Samia amesema hayo akihutubia viongozi mbalimbali wa dini katika Sherehe za kumpongeza Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi katika Jubilee ya Miaka 25 ya Utumishi wake wa Uaskofu leo tarehe 22 Februari, 2022 katika viwanja vya Posta Ngara mkoani Kagera.

Rais Samia alikuwa akijibu kauli iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi aliyemuomba Rais Samia kutokubali kulinganishwa na Mungu kwa namna yoyote ile na atajitahidi kuwa na hekima na uvumilivu na awe na sikio la kusikiliza yale yanayosemwa na wengine.

“Baba Askofu katika kufunga hotuba yako umeniasa mambo ya kukataa kutukuzwa na mimi nataka nikuahidi mbele ya umma huu kwamba, hii si tabia yangu na ninajitahidi kujishusha niwe sawa na wengine. Maana utumishi huu kama mipango ya Mungu ilivyo ameniweka hapa niwatumikie na siyo nijitukuze kwenu kwahiyo nitawatumikia,” amesema Rais Samia.

Rais Samia akiwa na Baraza la maaskofu Tanzania

Katika salamu zake kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara, Severine Niwemugizi Rais Samia akiungana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wamempongeza Askofu Severine Niwemuguzi kwa kuadhimisha Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu katika kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu.

Miaka hii 25 ya utumishi wa kiaskofu inafumbatwa na majitoleo mengi na utendaji wa Askofu Severine Niwemugizi katika eneo la Jimbo la Rulenge-Ngara, Kanisa la Tanzania na ulimwengu kwa ujumla katika kufundisha, kuongoza na kuwatakatifu watu wa Mungu ndani nje ya Tanzania.

Al-Shabaab wametumia zaidi ya bilioni 55 kununua silaha
Polisi wajawazito kufutwa kazi Nigeria