Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kushughulikia sakata la kupanda kwa gharama za vifurushi vya simu lililozua mjadala mzito kuanzia Aprili 2, 2021.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo, Aprili 6, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa taasisi na Idara mbalimbali aliowateua Aprili 4, 2021.

“Kuhusu suala la mabando kulizuka rapsharapsha juzi hapa, Wananchi wakapiga kelele mkalituliza, kalifanyieni kazi lisizuke namna ile mpo mnaangalia hawa watu wanakuja tu na mambo yao mpaka wananchi washtuke na nyie ndio mnashtuka, kakaeni na kampuni za simu,” amesema Rais Samia.

Young Africans yamvutia kasi Nado
KMC FC waisukia mipango Young Africans