Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila na kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa wawili.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chaalamila

Rais pia amemteua aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa Shinyanga, Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Batilda Salha Buriani

Hata hivyo Rais amefanya uhamisho wa Wakuu wa Mikoa wawili, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel anahamishiwa mkoani Mwanza kuchukua nafasi ya Chalamila huku Mkuu wa mkoa wa Tabora, Ally Happi akihamishiwa mkoa wa Mara kuchukua nafasi ya Mhandishi Robert Gabriel.

Taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa, Rais amemteua Zuwena Omar Jiri ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Tarehe ya uapisho wa viongozi hao itatangazwa baadae.

Aliyempiga kofi Rais Macron ahukumiwa kifungo cha miezi minne
Serikali yawasilisha makadirio ya Bajeti Kuu Ya Serikali ya mwaka 2021/2022