Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Baraza la maadili kusimamia sheria na kurekebisha maadili ya watenda kazi kwa kufanya kazi kwa bidii na kukuza maendeleo ya nchi hasa kiuchumi, huku akisistiza heshima katika utumishi wa umma kwa kutokuwa na heshima ya uwoga badala yake kuwa na heshima yakutoka moyoni.
“Tunasifiwa adjustement tulizofanya awamu ya tano kidogo zimekuza heshima ndani ya utumishi wa umma heshima iliyokuzwa ni heshima ya uwoga kwasababu kulikuwa na simba ya yuda ambaye ulikuwa ukishika sharubu zake anakurarua, lakini heshima inayotakiwa niya moyoni kila mmoja aheshimu majukumu ya mwenzake,” Amesema Rais Samia.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Aprili 2, 2022 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma wakati akiwaapisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri watatu kufuatia mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri aliyoyafanya hivi karibuni pamoja na Wajumbe wa Baraza la Maadili.
Amesema asingependa kuona Viongozi anaowateua wanafanya kazi kwa kufuata nafsi zao badala ya kuzingatia mipango ya nchi, irani, kukuza uchumi na dira ya nchi itakayomalizika 2025, huku akihainisha utendaji wa kazi kwa mtumishi wa umma asilimia 70 inampasa kufuata muongozo, sheria na dira, asilimia 30 kusikiliza nafsi lakini inayolenga malengo mazuri.
“Kwa ujumla kila mtu anajitazama, mimi niko hapa nakuaj, niko hapa natokaje , kwanza nitakaa miaka mingapi lakini nitatoka na nini ndicho tunachotazama hatutizami kwamba wajibu wangu ni kukuza nchi, wajibu wangu ni kukuza uchumi, wajibu wangu ni kuleta uimara wa taifa langu hatutizami hilo,” Amesema Rais Samia.
Aidha Rais Samia amewataka viongozi hao kuheshimu viapo walivyoapa kwa kufanya kazi kwa bidii na kutambua kuwa kazi kubwa iliyopo mbele ni kuhakikksha Taifa linapata maendeleo.