Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika dua maalum ya kumkumbuka Hayati Abeid Amani Karume, aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dua hiyo imefanyika katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM), zilizopo Kisiwandui, Zanzibar.

Mbali na Rais Samia, Viongozi wengine walioshiriki pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali.

Hayati Abeid Amani Karume aliuawa kwa kupigwa risasi April 7, 1972.

Mayay: Hawa jamaa ni hatari kwa sasa
Simba SC yawasili Cairo, Misri