Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein ametoa ufafanuzi juu ya mtazamo wa baadhi ya wananchi kudhania uchaguzi mkuu utaahirishwa kutokana na janga la corona kwa kubainisha kuwa uchaguzi lazima ufanyike.

Dkt. Shein amesema kuwa mipango ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu iko pale pale na Tume ya Uchaguzi itatangaza tarehe wakati utakapofika.

Aidha, akizungumzia uchumi wa Zanzibar amesema Serikali haijatetereka kiuchumi licha ya kuwepo kwa maradhi hayo na kila lililopangwa linatekelezwa ipasavyo.

Lakini ameongeza kuwa, yeyote aliyekuwa na nia ya kuisaidia Serikali anakaribishwa ila bila kuiwekea masharti kwani Serikali haiko tayari kusaidiwa kwa masharti.

Pamoja na hayo ameendeela kusisitiza kuwa hofu juu ya Ugonjwa huu ni mbaya sana hivyo, amewataka viongozi kuwaondoa hofu wananchi pamoja na kujiondoa hofu wao wenyewe

Watanzania 7 waliokwama Qatar kurejea
TFF yafafanua Dola za FIFA