Rais wa Shirikisho la Soka la nchini Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema hana mahaba na klabu ya Simba SC kama baadhi ya wadau wanavyodhani.


Karia amekua muhanga mkubwa wa kulaumiwa pindi yanapotoka maamuzi hasa yanayo zihusu klabu ya Simba SC na Young Africans.
Amesema mara nyingi amekuwa akishangazwa na madai ya wadau wa soka la Tanzania kumuhusisha sana na Simba SC, na badala yake amewataka wafahamu kuwa kanuni na taratibu ndizo huamua kutokana na kesi zinazofikishwa mbele ya Kamati za TFF, kuzihusu klabu hiyo kongwe nchini.


Hata hivyo hakusita kuitaja klabu anayoipenda kuwa ni Coastal Union ya Tanga ambako ndiko unyumbani kwao.


“Mimi kama ni mahaba ya timu yako Coatal Union na iko kubaya, inaishia shimoni, ila kusema nina mahaba na Simba inatoka wapi au naichukua Yanga kwa sababu gani.


“Mimi hata ugomvi na Young Africans sina, ni maneno ya watu tu, lakini katika maisha ukiwa kiongozi hauwezi kumfurahisha kila mtu na sio kwamba utendaji wangu utamfurahisha kila mtu, kuna mwingine nitamkera kutoka na utashi wake” amesema Karia.


Katika kipindi cha uongozi wa Karia kama Rais wa TFF, mashabiki na wanachama wa Young Africans wamekua wakiamini kila tatizo linalowakuta na kutolewa maamuzi, linasababishwa na kiongozi kwa kutia mkono.


Sakata la kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison, lilikua kilelezo kizuri kwa kiongozi huyo kudhihirisha ukweli wa chuki zilizojengeka baina yake na wanachama na mashabiki wa Young Africans, hasa baada ya Kamati kumuidhinisha mchezaji huyo kuwa huru na kujiunga na klabu yoyote.

Simba SC, Namungo FC zampa jeuri Bashungwa
Mwanafunzi wa chuo amnyonga mpenzi wake