Rais wa klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki, Fikret Orman ameonyesha nia ya kuona mshambuliaji kutoka nchini Italia na klabu ya Liverpool, Mario Balotelli anajiunga nao katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi,.

Orman amesema anaamini mshambuliaji huyo atawasaidia katika harakati zao za kusaka ubingwa wa nchini Uturuki kwenye msimu ujao wa ligi, endapo watamsajili.

“Mario Balotelli ni aina ya mchezaji ambaye tunamuhitaji na ninaamini hata mashabiki wetu wanampenda.

“Nitajitahidi kutoa ushawishi kwa viongozi wenzangu ili kufanikisha hatua ya kumsajili Balotelli.

“Kwa kweli ana matatizo yake binafsi ya kutokua na nidhamu anapokua nje na ndani ya uwanja, lakini nina uhakika jambo hilo linarekebishika endapo atapata watu sahihi wa kumuongoza, hivyo suala hilo kwetu sio tatizo kabisa. Alisema Fikret Orman

Balotelli kwa sasa anasaka klabu ya kuitumikia kuanzia msimu ujao, baada ya kuarifiwa na meneja wa klabu ya Liverpool, hana nafasi katika kikosi chake.

Bila Pauni Milion 40, Lacazette Hang'oki Lyon
Azam FC Wafanyishwa Mazoezi Kwenye Maji