Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amesaini muswada wa sheria unaohalalisha matumizi ya dawa za kulevya zinazotokana na mimea asilia ikiwa ni pamoja na bangi.

Akitangaza uamuzi huo kupitia Televisheni ya Taifa, Rais Santos alieleza kuwa hivi sasa ni halali kwa mtu yeyote kustawisha, kuchakata, kuingiza au kutoa nchini humo bangi kwa matumizi ya kisayansi au tiba.

“Hii inaifanya Colombia kuwa kati ya nchi zilizo mstari wa mbele kutumia rasilimali asilia katika kupambana na magonjwa,” alisema Rais Santos na kuongeza kuwa hatua hiyo haitaenda kinyume na nia yao ya kuungana na mataifa kupambana na matumizi ya dawa za kulevya.

 

Baada ya Ushindi Wake Kubatilishwa Ndani ya Dakika Chache, Miss Colombia Atoa Fundo Moyoni
Pius Msekwa adaiwa kudanganya Kuhusu Stori yake na Mwalimu Nyerere