Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino amemwahidi Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuwa FIFA itawekeza katika miradi ya maendeleo ya soka nchini.

Infantino ametoa ahadi hiyo jana katika mazungumzo yake maalum na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake baada ya kumtembelea ikiwa ni sehemu ya ratiba zake nchini baada ya kumaliza mkutano mkuu wa FIFA wa mwaka wa kikanda.

Aidha, Rais huyo aliyechukua mikoba ya Sepp Blatter Februari 26 mwaka 2016 ameunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kupambana na rushwa katika sekta ya michezo.

Infantino ameishukuru Serikali kwa ukarimu wake na kumuomba Waziri Mkuu kufikisha salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mapokezi mazuri.

Hata hivyo, kwa upande wake Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Tanzania inaunga mkono juhudi za FIFA katika kupambana na rushwa kwenye soka pamoja na matumizi mabaya ya fedha na madaraka.

 

Aslay na Nandy wapigwa faini milioni 5
Kiongozi wa upinzani ang’atuka kugombea urais