Wakati Umoja wa mataifa na Marekani wakizidi kupinga vikali utengenezaji wa silaha za nyuklia Rais wa Iran amesema kuwa nchi yake itaunda silaha zozote inazohitaji ili kujilinda dhidi ya uvamizi.

Wakati akihutubia bunge Rais Hassan Rouhani amesema kuwa Iran haitakuwa ikikiuka makubaliano yoyote ya kimataifa kwa kutengeneza silaha yakiwemo makombora ya masafa marefu.

Rais huyo aliionya Marekani kuwa ukiukaji wa mkataba wa nyuklia uliotiwa sahihi kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu ni kwa manufaa yake.

Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibuni alikataa kuidhinisha mkataba huo akiitaja Iran kama nchi kaidi inayounga mkono ugaidi.

Daxo Chali awatimua wasanii wake wa kike kwa ‘kuchepuka’ na Nay wa Mitego
Bila kisu kikali huwapati wachezaji hawa Uingereza