Rais mteule wa Liberia, George Oppong Weah, ametangaza kupunguza mshahara wake kwa asilimia 25 ili atimize sehemu ya mpango wake wa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.
Mwanasoka huyo nguli duniani ambaye aliapishwa kuwa raisi hivi karibuni amesema kuwa ameamua kupunguza mshahara wake ili fedha hizo ziende kusaidia shughuli zingine za uchumi.
Aidha, Liberia kwa sasa inakabiliwa na changamoto za kiuchumi ikiwemo kupanda kwa gharama za maisha na vijana wengi kukosa ajira.
Hata hivyo, Weah,amechukuwa madaraka kutoka kwa aliyekuwa raisi wa kwanza mwanamke barani Afrika, Ellen Johnson Sirleaf, aliyechaguliwa mwaka 2006 na baadaye 2011 kuchaguliwa kwa mara ya pili, ambapo kabla ya kuiongoza nchi hiyo ilikuwa kwanye vita ya wenyewe kwa wenyewe.