Rais wa Marekani Joe Biden leo Agosti 31 anatarajia kulihutubia Taifa baada ya siku 17 za ukoaji wa raia wa Marekani pamoja na wanajeshi wake nchini Afghanstan.
Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa fupi ya kuwashukuru wale wote waliohusika katika operesheni ya uokoaji tangu Taliban ilipofanikisha kuchukua nchi ya Afghanstan.
Hata hivyo Jeshi la Marekani limetangaza kukamilika kwa shughuli ya kujiondoa Afghanistani, Ndege ya mwisho ya jeshi la Marekani imeondoka Kabul, ikiashiria mwisho wa uwepo wa nchi hiyo nchini Afghanistan.
Aidha Kamanda Mkuu wa Jeshi la Marekani, Jenerali Kenneth McKenzie, amesema ndege ya mwisho ya C17 imeondoka Kabul ikiwa na balozi wa Marekani.
Kuondoka kwa ndege hiyo ya mwisho kunaashiria kumalizika kwa vita virefu kabisa vya Marekani ambapo juhudi kubwa ya uokoaji ilianza Agosti 14 mara tu baada ya Taliban kuchukua nchi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken amesema kuwa moja ya changamoto amabayo nchi ya Marekani imewahi kuipati katika utekelezaji wake ni pamoja na uhamisho huo katika nuanja ya kijeshi, kidiplomasia na kibinadamu.
“Ukurasa mpya umeanza Ujumbe wa kijeshi umekwisha. Ujumbe mpya wa kidiplomasia umeanza.” Amesema Blinken.
Baada ya ndege ya Marekani kuondoka ilisikika milio ya bunduki hewani ikipigwa na Taliban kama ishara ya kushangalia kuondoka kwa majeshi hayo