Rais wa Myanmar, Htin Kyaw amejiuzulu nafasi hiyo kwa sababu zilizotajwa kuwa za kiafya.
Uamuzi huo umeripotiwa wakati ambapo Kansela wa taifa hilo, Aung San Suu Kyi anashinikizwa na Umoja wa Mataifa kutoa ufafanuzi kuhusu kampeni za vurugu zilizofanywa na jeshi katika jimbo la Rakhine.
Ripoti zimeeleza kuwa Kyaw mwenye umri wa miaka 71 alikuwa mgonjwa kwa miezi kadhaa.
Ofisi ya Kansela imesisitiza kuwa uamuzi wake wa kujiuzulu umetokana na kufanyiwa upasuaji mara kadhaa.
Htin Kyaw alikuwa rais wa kwanza wa Myanmar asiyefungamana na jesh, tangu mapinduzi ya mwaka 1962.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, nafasi yake itashikiliwa na aliyekuwa makamu wake, Myint Swe ambaye ameteuliwa na jeshi.