Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas(Abu Mazen), amempinga hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyohutubia katika kikao na uongozi wa Palestina ambacho lengo lake kuu ni kujadili na kutoa majibu kwa uamuzi wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalemu.
Rais Abbas ameielezea hatua hiyo kama pigo la karne akinukuu matamshi ya Rais Trump mwenyewe juu ya maelezo ya mpango mkubwa wa amani wa Marekani kama mpango wa karne.
Aidha, Rais Abbas amesha toa tamko kuwa Wapalestina hawatashiriki tena katika mpango wowote wa Marekani kufuatia Rais Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel
Chanzo kikuu cha mzozo huo kati ya Marekani na Palestina ni baada ya Rais Trump kutangaza kuwa mji wa Yerusalem ndio mjii mkuu wa Israel ambapo kufuatia tangazo hilo la Trump, Rais wa Palestina, Abbas amesema kuwa hawezi kamwe kukubali mpango wowote wa amani wa Marekani kufuatia hatua hiyo ya Trump.
Maandamano yalizuka katika ukanda wa Gaza baada ya tangazo hilo.
Wapalestina 13 wameuawa kwenye ghasia kufuatia tangazo hilo la Trump wengi wakiuawa wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Israel.
Israel na Palestina wamekuwa wakizozana kutokana na mji wa Jerusalem, Israel ilitwaa eneo la mashariki mwa mji, ambalo awali likuwa linakaliwa na Jordan wakati wa vita vya mwaka 1967 vya masahariki ya kati na inadai kuwa mji huo wote ni wake.