Taarifa kwa umma

Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva anayo furaha kubwa ya kuwatakia waislaam wote nchini maandalizi mema ya nguzo ya nne ya dini ya kiislaam kufunga swaumu ya Ramadhan…

Katika salaam zake za ibada hiyo muhimu rais Aveva amewaomba wanachama na washabiki wa Simba kutumia ‘fardhi’ hiyo muhimu kuendelea kuiombea klabu ambayo ipo kwenye mchakato muhimu wa usajili wa wachezaji na pia maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka utakaofanyika mwezi ujao tarehe kumi…

Kwenye salaam hizo pia amewaomba waislaam kuongeza ibada kwa mola wao kama walivyoamrishwa katika kitabu kitukufu cha Qur-ani.

…ni matumaini yangu kuwa Ramadhani hii itaendelea kutuunganisha wanasimba na wapenda michezo kote nchini…alimalizia rais.kwenye salaam zake hizo.

Imetolewa na
Haji S.Manara
Mkuu wa habari
Simba sports club

Simba nguvu moja

Philippe Coutinho Azigonganisha FC Barcelona, Paris Saint-Germain
Zlatan Ibrahimovic Kumalizana Na Man Utd Kesho