Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa amewasili nchini leo mchana na kupokelewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

Sheikh Salman amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili na atakua na mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Kesho Jumanne, Sheikh Salman Bin Ebrahim Ali Khalifa atamtembelea ofisini Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel.

 

Tuhuma Za Upangaji Wa Matokeo Kwenye Tennis
Picha: Waliokumbwa na Bomobomoa Mkwajuni wafunga barabara na kufanya fujo