Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed amesaini Sheria Tata inayoongeza mamlaka yake kwa miaka miwili, huku hatua hiyo ikipingwa vikali na Wafadhili.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Serikali na Waziri wa Habari, Osman Dubbe, Rais amesaini Sheria hiyo ambayo ilipitishwa na Bunge.

Hata hivyo Seneti ilipinga hatua hiyo ikisema ni kinyume na Katiba.

Muda wa Urais wa Rais Abdullahi ulifika tamati mwezi Februari mwaka huu bila kupatikana Mrithi wa nafasi hiyo.

Wafadhili wakubwa wa Taifa hilo wamesisitiza hawataunga mkono suala la Rais kuongezewa muda.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 15, 2021
Biden kuondoa jeshi la Marekani Afghanistan