Rais wa Ufaransa Emanuel Macron, ametoa majibu yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu juu ya madai ya  waandamanaji wa vizibao vya njao katika nchi yake.

Macron ameahidi kupunguza ada ya kodi katika mafuta, kuwalipa mafao makubwa na kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi wa serikalini.

Aidha amesema kuwa anayatambua maandamano hayo yaliyo dumu kwa muda wa miezi mitano kuwa chanzo chake kilikuwa na madai ya haki.

Uamuzi huo ameutoa katika hotuba yake ambayo hapo awali ilipangwa kufanyika April 15, lakini ilisogezwa mbele baada ya  nchi hiyo kukumbwa na janga la moto ulioteketeza kanisa la kihistoria.

Waandamanaji wa vizibao vya njano licha ya kupinga vikali upandaji wa bei ya mafuta, walikuwa wanapinga pia kutokuwa na haki katika maendeleo ya uchumi wa taifa lao.

kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa amesema kuwa amejifunza mengi na kujua wananchi wake wanataka nini kupitia mijadala mbali mbali ya kitaifa iliyokuwa inafanywa na wananchi kueleza ni mabadiliko gani yafanyike.

Rais Macron alipo chaguliwa mwaka 2017, aliapa kupigania na kupinga nguvu ya mgawanyo ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya Ufaransa na watu wake.

 

 

 

 

 

 

“Pogba hataki kuwa Manchester United”
Kim Jong Un aishushia tuhuma Marekani, ahamia kwa Putin