Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amepigwa kibao cha uso na kijana mmoja alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini humo.

Video inayosambaa katika mitandao ya kijamii inamuonyesha Macron akitembea kuelekea katika sehemu waliyokuwepo wananchi ambapo kijana mmoja anaonekana akimshambulia Kiongozi huyo na baadaye maofisa usalama walimuondoa kiongozi huyo na kumpeleka eneo lenye usalama.

Baada ya tukio hilo video inamuonyesha Macron akirejea tena katika eneo la tukio na kuendelea kuwasalimia watu wengine.

Tukio hili limetokea wakati Macro alipolitembelea eneo la Drome Mashariki mwa Ufaransa ambako alikutana na wamiliki wa migahawa na wanafunzi kuzungumza nao kuhusu jinsi maisha yanavyorejea hali ya kawaida baada ya janga la Covid-19.

Hadi sasa haijafahamika ni kwanini kijana huyo alifanya kitendo hicho, taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya nchi hiyo inasema vijana wawili wanashikiliwa na polisi kutokana na tukio hilo.

Tukio kama hilo liliwahi kutokea hapa Tanzania Machi 10, 2009 baada ya kijana Ibrahim Said, kumzaba kofi Rais mstaafu Alli Hassan Mwinyi aliyekuwa akiwataka Waislamu kutumia kondomu kujikinga na Ukimwi.

Rais Samia afanya uteuzi
Kakolanya kusalia Simba