Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron anatarajiwa kufanya ziara nchini Rwanda Mei 27,2021 ziara inayoangaziwa kufungua ukurasa mpya wa historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Macron atakuwa Rais wa pili wa Ufaransa kutembelea Rwanda baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 tangu rais wa zamani Nicolas Sarkozy alipotembelea taifa hilo mnamo 2010.

Rwanda ilivunja uhusiano wake na Ufaransa mwaka 2006 kwa shutuma za mauaji ya kimbari.

Ziara ya Macron nchini Rwanda imeelezwa na mashirika ya manusura wa mauaji ya kimbari kuwa ishara nzuri katika kuweka mambo sawa.

Mwenyekiti wa shirika la manusura la IBUKA, Egide Nkuranga amesema hiyo ni ziara ya matumaini kuwa hatimaye huenda waliofanya mauaji ya kimbari na kukimbilia Ufaransa watashikwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

‘Tunachosubiri kwa ziara ya Bwana Macron ni kutoa haki ya sheria kwa manusura wa mauaji ya kimbari kwa kuwakamata waliohusika na kuwafikisha mahakamani,”amesema Nkuranga .

Ubelgiji, Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa ziliomba radhi kwa kushindwa kusaidia kukomesha mauaji ya kimbari.

Kennedy asaini miwili Simba SC
Gomes ampotezea wakala wa Kagere