Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte (76) amesema anajiuzulu siasa na hatagombea katika uchaguzi wa mwakani (2022) katiba ya nchi hiyo inawaruhusu marais kuhudumu muhula mmoja wa miaka sita.

Hatua hii inakuja huku kukiwa na uvumi kuwa binti yake anaweza kugombea urais Sara Duterte-Carpio, ambaye kwa sasa ni meya wa mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Davao.

Duterte anasema ameamua kujiondoa kwenye uchaguzi wa mwakani kwani “hisia za Wafilipino wengi ni kwamba hafai kuongoza tena.

Rais Duterte, aliingia madarakani mwaka 2016 ambapo aliahidi kupunguza uhalifu na kutatua mzozo wa madawa ya kulevya nchini humo.

Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka mitano akiwa maadarakani  Duterte amewachochea polisi kufanya mauaji ya ukiukaji wa sheria ya washukiwa katika kile alichokiita “vita dhidi ya madawa ya kulevya ”

Trilioni 5.151 zakusanywa robo ya kwanza mwaka wa fedha
RC Mbeya awapa angalizo wazee kuitwa 'bebi'