Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amelazwa hospitalini baada ya kuambukizwa virusi vya Corona mapema wiki hii.

Taarifa hii imethibitishwa na msemaji wa ofisi ya rais ambaye amesema “Kwanza alikwenda nyumbani, lakini aliamua kwenda Feofania (hospitali). Ili kujitenga na watu.”

Aidha amesema kuwa hali ya rais ni nzuri, pia ameeleza kuwa hali za wagonjwa wote ni nzuri hakuna mwenye hali mbaya.

Siku ya Jumatatu Zelenskiy alisema kuwa alipima na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona, wakati maafisa wengine watatu wa juu, pamoja na waziri wa fedha, waziri wa ulinzi na msaidizi mkuu wa Zalenskiy pia waliripotiwa kuambukizwa COVID-19.

Idadi ya maambukizi mapya ya virusi vya corona nchini Ukraine ilianza kuongezeka mwishoni mwa Septemba na imekuwa ikiongezeka mwezi Oktoba na Novemba, ikiichochea serikali kuongeza vizuizi kadhaa hadi mwisho wa mwaka.

Siku ya Jumatano, baraza la mawaziri la Zelenskiy lilipiga kura ya kuweka kizuizi cha kitaifa mwishoni mwa wiki, ili kuimarisha hatua za kuzuia kuenea kwa kasi kwa virusi vya Corona.

Hadi sasa, Ukraine imetangaza jumla ya visa 500,865 vya Covid-19, na vifo 9,145.

Serikali ya Zimbabwe yatishia kuwafukuza kazi walimu waliokataa nyongeza ya mishahara
Bunge lawakubali Majaliwa, Tulia