Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ameitaka Saudi Arabia kueleza mahali ulipo mwili wa mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi aliyeuwawa katika ubalozi mdogo wa Saudia nchini Uturuki.
Pia amewataka wamtaje mtu aliyetorosha mwili wa mwandishi huyo, baada ya kuuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, nchini Uturuki.
Aidha, wakati akikutana na wanachama wa chama chake cha (AK) bungeni, Edorgan amesema kuwa, Ankara ina ushahidi kuhusiana na mauaji ya mwandishi Khashoggi, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Edorgan amesema kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa Saudi Arabia, atatembelea Istanbul siku ya Jumapili ili kukutana na maafisa wa Uturuki kama sehemu ya uchunguzi wake.
Pia Saudi Arabia imekiri kwamba mauaji ya Khashoggi yalipangwa kwa kuzingatia ushahidi ambao umetolewa na Uturuki.
Hata hivyo, jambo lisilo julikana ni nani walio muua mwandishi huyo, ambapo mpaka sasa washukiwa 18 tayari wameshakamatwa nchini Saudi Arabia.