Rais wa Yemen aliyekuwa uhamishoni amemfuta kazi makamu wake, kisha akajiuzulu, na kukabidhi madaraka kwa baraza la rais kwa lengo la kuanzisha mazungumzo yanayo lenga kumaliza mzozo wa miaka saba nchini humo.
Rais anayemaliza muda wake Abed Rabbo Mansour Hadi aliashiria kampeni inayoongozwa na Saudia kumaliza uasi wa Houthi imeshindikana kwa kumfuta kazi Makamu wa Rais Ali Mohsen al-Ahmar, kamanda wa jeshi ambaye aliteuliwa mwaka 2016 kuongoza mashambulizi ya ardhini ambayo yamefikia ukomo.
Kuondoka kwao kunaweza kuimarisha usitishaji vita wa miezi miwili uliokubaliwa mwanzoni mwa mwezi huu na serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia na waasi wa Houthi, usuluhishi wa kwanza tangu 2016, na kurejesha juhudi za kuleta amani ambazo zimekwama katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Tayari makundi yanayohasimiana yameridhia kusitisha vita kwa miezi miwili kuanzia jumamosi ijayo.
Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ambazo zina dhima kubwa katika vita hivyo zinaonesha kuhusika na uamuzi wa rais Mansour Hadi na zimekuwa wa mwanzo kuupongeza na kutoa ahadi ya kuchangia msaada wa dola bilioni 3.
Aliyeteuliwa kuliongoza baraza hilo jipya la uongozi ni mtu mwenye mafungamano ya karibu ya serikali ya mjini Riyadh.
Kupitia ujumbe wa Tweeter mjumbe wa ngazi ya juu wa Kundi la Houthi Mohammed Abdul-Salam ameupuuza uteuzi wa baraza hilo jipya