Rais wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu,ambapo Kifo chake kimetangazwa na televisheni ya taifa kufuatia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa nchi hiyo
Bouteflika ameongoza nchi hiyo kwa karibu miongo miwili na kuachia madaraka mwaka 2019 baada ya jaribio lake la kugombea muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa.
Hata hivyo kiongozi huyo ndo kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi nchini humo, alikuwa kiungo muhimu katika vita vya kupigania uhuru wa Algeria miaka ya 1950 na 60, akiwa na umri wa miaka 25, aliteuliwa kuwa Waziri wa kwanza wa Mambo ya Nje wa taifa hilo baada ya kujipatia uhuru kutoka kwa Ufaransa.
Bouteflika alisaidia kuituliza na kuiunganisha nchi yake iliyoharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyogharimu maisha ya takribani watu 200,000 katika miaka ya 1990.
Aidha Mwaka 2013, Bouteflika aliugua kiharusi na alionekana kwa nadra hadharani – hali iliyozusha uvumi kuhusu afya yake kwa miaka kadhaa.