Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka tisa na nusu baada ya kesi tano za ulaji rushwa zilizokuwa zikimkabili kutolewa hukumu huku zingine zkiwa bado kutolewa maamuzi.
Rais huyo wa zamani wa Brazil alijitajirisha mara baada ya kupata nafasi hiyo na kuwa miongoni mwa marais maarufu duniani huku akitumia nafasi hiyo kujitajirisha kwa kujilimbikizia mali.
Aidha, Rais huyo wa zamani wa nchi hiyo alijizolea umaarufu kutokana na sera zake za kusaidia jamii ya watu masikini nchini mwake kitu ambacho kiliungwa mkono na nchi mbalimbali duniani.
Lula kwa sasa mambo yamemgeukia kwa kukutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.
Vilevile hukumu hiyo imekuja mara baada ya rais huyo kutangaza kugombea kuingia katika kinyang’anyiro cha nafasi ya urais mwakani hivyo kuonyesha msimamo mkali kuhusiana na hukumu hiyo.
Hata hivyo, wakati huo huo Kamati ya Bunge la Congress la Brazil linajadili iwapo iiruhusu mahakama kusikiliza kesi inayomkabili rais wa sasa wa Brazil, Michael Temer kuhusiana na tuhuma inayomkabili.