Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak amefariki dunia baada ya kuugua na kufanyiwa upasuaji.
Rais huyo aliyeiongoza Misri kwa miaka 30 kabla ya kutolewa madarakani kwa maandamano yaliyofanyika mwaka 2011 amefariki akiwa na miaka 91.
Rais huyo aliyeingia madarakani mwaka 1981 akiwa Rais wa nne wa nchi hiyo, amefariki dunia akiwa katika Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU) wiki kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji.
Alifungwa kwa miaka kadhaa baada ya ghasia zilizomuondoa madarakani, lakini mwaka 2017 aliachiwa huru baada ya kutokutwa na hatia katika mashtaka yake mengi.