Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amehudumu kama Kiongozi wa nchi kwa kipindi cha miezi minane bila malipo tangu achukue hatamu za uongozi wa nchi hiyo mnamo Agosti 2021.

Kwa mujibu wa Shirika la Jabari la Al Jazeera, Rais huyo alisema mshahara wake haukuwa motisha yake kuwania wadhifa huo na kuongeza kuwa ameamua kukataa malipo hayo kwa sababu ya masilahi ya umma.

“Suala la mshahara si suala la msingi kwa sababu pesa haikuwa msukumo wetu wa kutafuta ofisi ya umma na sio kwamba serikali haikuwa tayari kulipa, ni kwamba sijazingatia mshahara huo wa rais,” aliwaambia waandishi wa habari.

Uamuzi wake wa kukataa kulipwa mshahara hadi sasa umezua hisia tofauti huku baadhi ya Wazambia wakitaja kitendo chake kuwa cha kibinadamu, huku wengine wakisema hastahili kulipwa kabisa kwa sababu bado hajatimiza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni.

Baadhi ya watuamiaji wa Mitandao wametoa maoni yao “Nina uhakika ana njia nyingine ya kuzalisha na kupata pesa kwa benki. Siwaamini viongozi wa Afrika. Kukaa miezi minane bila mshahara kunaweza kuwa na maana ikiwa alikuwa akilipa gharama za kila siku kutoka mfukoni mwake,”

“Natamani angekuwa kiongozi wetu Tanzania. Nchi nyingine zinahitaji kiongozi wetu awe wao,” mwingine alibainisha.

Hichilema hajapokea mshahara kwa Miezi 8 tangu alipomshinda mpinzani wake mkuu, Edgar Lungu, baada ya kupata kura milioni 2.8 katika uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali mwezi Agosti akiwania kiti hicho kwa mara ya tano.

Rais wa Ukraine kufanya kikao na Rais wa Halmashauri kuu ya Ulaya
Mabinti wa Putin wawekewa vikwazo Marekani