Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amenusurika kifo baada ya kutokea mlipuko wa bomu kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika mapema leo jijini Bulawayo.
Mnangagwa amesema kuwa mlipuko huo ulishambulia inchi kadhaa kutoka eneo alilokuwa amekaa, lakini siku zake zilikuwa hazijafika.
Kipande cha video ya tukio hilo kinaonesha mlipuko ukitokea karibu na alipokuwa Rais huyo, sekunde chache baada ya kutoka jukwaani kuomba kura.
“Asubuhi hii tulikuwa tunafanya kampeni nzuri jijini Bulawayo. Kulikuwa na mlipuko jukwaani. Watu kadhaa walijeruhiwa na mlipuko huo, na tayari nimefika kuwajulia hali hospitalini,” inasomeka tweet yake kwa tafsiri isiyo rasmi.
This afternoon, as we were leaving a wonderful rally in Bulawayo, there was an explosion on the stage. Several people were affected by the blast, and I have already been to visit them in the hospital.
— President of Zimbabwe (@edmnangagwa) June 23, 2018
Waziri wa Afya, David Parirenyatwa amesema kuwa watu 15 wamejeruhiwa, ambapo kati yao watatu wako katika hali mbaya kutokana na mlipuko wa bomu hilo. Bado idadi kamili ya majeruhi haijawekwa wazi.
Mnangagwa na viongozi wengine wa chama cha Zanu-PF walikuwa jijini Bulawayo, jiji la pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe na ngome kuu ya upinzani, ikiwa ni sehemu ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Julai 30 mwaka huu.
Makonda aweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi
Ingawa anatarajiwa kushinda uchaguzi huo, anakabiliwa na maadui wengi kufuatia mchakato wa kuingia madarakani baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe kuondolewa kwa shinikizo la kijeshi.
- Makonda aweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi
- RC Katavi atangaza fursa kiwanja cha ndege Mpanda
Msemaji wa Rais Mnangagwa amesema kuwa hakupata madhara yoyote kwenye tukio hilo lakini Makamu wa Rais, Constantino Chiwenga anadaiwa kupata mikwaruzo usoni.
Chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika.