Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema kuwa anahisi kundi la G40 linalomuunga mkono mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe linahusika na tukio la mlipuko wa bomu kwenye mkutano wake.
Mnangagwa amemwambia wandishi wa BBC kuwa anaamini kuwa bomu hilo lililolenga kumuua kwenye mkutano huo linauhusiano na kundi hilo kutokana na mgogoro wa nafasi ya urais kupitia chama cha Zanu-PF kati yake na Mama Grace.
“Sijui kama mtu mmoja anaweza kufanya hili. Nafikiri itakuwa ni njama ya zaidi ya mtu mmoja. Na nadhani chanzo ni tukio la kisiasa linafanywa na watu ambao wamechukizwa na uwepo wangu,” alisema.
“Nitamuamini vipi mtu ambaye mara kadhaa amekuwa akinishambulia kwa maneno bila sababu za msingi,” aliongeza.
Mama Grace aliwahi kueleza kuwa adui wa Mugabe ni Mnangagwa ambaye alikuwa makamu wa rais.
Mnangagwa aliingia madarakani kufuatia shinikizo la kijeshi lililosababisha Mugabe kujiuzulu. Fukuto la mgogoro ndani ya ZANU-Pf lililoambatana na tetesi kuwa mama Grace anataka kuachiwa nafasi ya urais ni sababu kubwa iliyosababisha mabadiliko ya madaraka mwaka jana.
- Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 27, 2018
- Video: Kauli za wabunge mwiba kwa Dk. Mpango, Mawaziri nao ndani wadaiwa sugu JWTZ
Serikali imetangaza msako mkali dhidi ya watu waliohusika na tukio hilo ikiwa imebaki mwezi mmoja taifa hilo lifanye uchaguzi mkuu.