Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa anatazamiwa kuzindua Bunge ndani ya Jengo jipya lenye viti 650 jijini Harare ambalo limejengwa na kampuni ya kutoka China na kutumia fursa hiyo kutoa hotuba yake kuhusu hali ya nchi.

Hotuba ya kiongozi huyo, itafuatwa na ya Waziri wa Fedha ambaye atasoma bajeti ya kitaifa ya 2023, ya ripoti inasema kwamba ujenzi huo ulianza mwaka wa 2018, na kwamba usanifu huo unachanganya sifa za jadi za Zimbabwe na Kichina.

China, ilifadhili mradi huo wa ujenzi wa Bunge la Kitaifa na Seneti kama zawadi kwa Zimbabwe na liko kilomita 18 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Harare ambapo Kampuni ya Ujenzi ya Construction Group (SCG) ilisema jengo hilo ni la kihistoria na dhihirisho ya urafiki wa China na Zimbabwe. .

Sehemu ya viti katika Jengo jipya la Bunge la Kitaifa nchini Zimbabwe lenye viti 650. Picha ya Xinhua.

SCG, ilikamilisha majengo hayo katika muda wa miezi 42, na kuchelewa kwa miezi 10 nyuma ya ratiba huku ucheleweshaji ukihusishwa na kuzuka kwa janga la Covid-19.

Haya yanajiri, huku mataifa mengi barani Afrika yakiendelea kuzongwa na madeni na mikopo ya China. Zimbabwe, ambayo ina deni kubwa ya China, bado inategemea nchi hiyo ambayo iko tayari kutoa mikopo kwa Harare kutokana na rekodi yake mbaya ya ulipaji madeni.

Wakati wa utawala wa Hayati, Robert Mugabe Zimbabwe iliathirika vibaya uchumi kutokana na kutengwa na kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi kuhusiana na madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na udanganyifu katika uchaguzi.

Lionel Messi: Hii ni nafasi yangu ya mwisho
Korea Kaskazini kuandaa Fainali za Kombe la Dunia