Mahakama ya Rufaa ya jiji la Bangui Nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati – CAR, imemuhukumu Rais wa zamani wa Taifa hilo, Francois Bozize kifungo cha maisha jela na kazi ngumu kwa kupatikana na makosa ya kula njama, kuhatarisha usalama wa ndani, uasi na mauaji.

Bozize anayeishi uhamishoni Nchini Chad, aliyechukua mamlaka ya kuiongoza CAR mwaka 2003 na kupinduliwa muongo mmoja baadaye, alihukumiwa bila kuwepo mahakamani siku ya Alhamisi Septemba 21, 2023 na anadaiwa kwasasa anaongoza Muungano wa waasi.

Rais wa zamani wa CAR, Francois Bozize. Picha ya WANE 15.

Mbali na Bozize, pia Watoto wake wawili wa kiume na washtakiwa wengine 20, ambao ni pamoja na Viongozi wa waasi nao walipewa hukumu hiyo bila kuwepo Mahakamani akimemo na Kiongozi wa Kijeshi wa Kundi Kuu la Wanamgambo ndani ya Muungano wa CPC, Ali Darassa.

Bozize (76), mpaka mwezi Machi wakati alipohamia Guinea Bissau anaongoza muungano wa makundi ya waasi yanayoitwa Coalition of Patriots for Change (CPC), yaliyoundwa Desemba 2020 kwa nia ya kumpindua mrithi wake, Faustin Archange Touadera.

Mkuu wa Mkoa wa zamani ashitakiwa kwa mauaji
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 24, 2023