Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewafanyia ‘suprise’ ya kuwatembelea wanajeshi wake waliopo katika mji wa Izium kaskazini uliopo mashariki mwa nchi hiyo, huku kitendo hicho kikitafsiriwa ni kuyahatarisha maisha yake.

Mji huo wa Izium, ulikombolewa hivi karibuni kutoka mikononi mwa wapiganaji wa Urusi, ikiwa ni ishara dhahiri ya kuongezeka kwa ari ya Ukraine na imani yake katika kuwa na jeshi linaloweza kuhakikisha usalama wa kiongozi wake katika ukanda wa vita.

Katika miji ya Kirusi iliyo karibu na mapigano, hali imekuwa ni ya wasiwasi hasa eneo la Belgorod lililopo umbali wa maili 25 kutoka mpaka wa Ukraine huku sauti za milipuko ya karibu zikiwa ni matukio ya kawaida.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine, akisalimiana na Wanajeshi huko Izium. Picha na Nicole Tung wa The New York Times.

Malori ya kijeshi yaliyowabeba wanajeshi waliojihami kwa rangi ya herufi Z, yamekuwa yakipishana kwenye makutano, na wakimbizi wanaendela kumiminika kutoka maeneo ya Ukraine.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amejaribu kuweka maisha kuwa ya kawaida kwa Warusi wengi wa maeneo jirani na mapambano, kwa kufanya uhasama wake na nchi yaUkraine kuonekana ni dhana ya mbali.

Hata hivyo, kwa kuwa vikosi vya Ukraine sasa vinashambulia maeneo jirani na Urusi, wakaazi wengine wa eneo jirani la Belgorod wanahisi kuwa tayari vita vimewafikia.

Serikali yatahadharisha uwepo wa Surua nchini
Tahadhari yatolewa mfululizo wa mvua kwa miezi sita