Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya vijana yatakayofanyika Oktoba 14 mkoani simiyu.

Hayo yamesemwa na  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam

Mhe Mavunde amebainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija


Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hiyo ni kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.

 Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali kama makongamano,ma tamasha,michezo,maonyesho ya Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.

“Tanzania itasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hiyo itaenda sambamba na Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.

Wazo la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Akimbizwa hospitali baada ya kukaa ‘Airport’ siku 10 akimsubiri mpenzi aliyempata Mtandaoni
Kanumba Star Search Yazinduliwa