Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho” amefichua kuwa licha ya kuwa na mchezo mgumu dhidi ya Coastal Union lakini kwa upande wake bado anapambana kujenga mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kufuatia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Power Dynamo ya Zambia.
Robertinho ametoa kauli hiyo kuelekea katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga unaotarajia kupigwa kesho Alhamisi (Septamba 21) kwenye Uwanja wa Azam Complex, kabla ya kuwavaa Power Dynamo katika mchezo wa pili wa hatua ya pili wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Robertinho amesema kuwa amepanga kuutumia mchezo wa na Coastal Union kurekebisha makosa yaliojitokeza kwenye michuano ya Ligi ya Mabigwa Barani Afrika kabla ya mchezo wa marudiano utaopigwa nchini.
Robertinho amesema kuwa ameona mapungufu ya kikosi chake huku akifurahishwa waliocheza kipindi cha pili hali iliopelekea kupanga mikakati mengine katika mchezo wao dhidi ya Coastal kabla ya kuwavaa Power Dynamos.
“Tumerejea nyumbani kuendelea na programu ya maandalizi ya mechi yetu ijayo, nitakuja na mbinu mpya ambayo itaanza kufanyia kazi dhidi ya Coastal Union kwa ajili ya maandalizi yetu ya mechi ijayo ya marudiano ya ligi ya Mabingwa Afrika.
“Nimefurahishwa na kipindi cha pili walivyocheza ukiangalia Fabrice Ngoma, Luis Miquissone, Jean Baleke na Saido Ntibazonkiza wamecheza vizuri mechi iliyopita lakini ni muda wa kufanyia kazi changamoto zilizojitokeza Zambia,” amesema Robertinho.