Mwenyekiti wa Chama Tawala Nchini Afrika ya Kusini (ANC), Cyril Ramaphosa amepishwa kuwa rais wa nchi hiyo mara baada ya rais wa taifa hilo Jacob Zuma kujiuzulu.
Rais huyo mpya alikuwa mtu pekee aliyeteuliwa kugombea nafasi hiyo, ambapo uteuzi huo uliungwa mkono kwa asilimia kubwa ya wabunge.
Aidha, aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma alikuwa anakabiliwa na shinikizo kali ndani ya chama chake cha ANC kilichomtaka ajiuzulu, huku kikitishia kupiga kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.
Hata hivyo, Zuma anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya ufisadi lakini amekana kufanya makosa yoyote, huku akisema hakubaliani na maamuzi ya chake.