Beki wa kati kutoka nchini Hispania, Sergio Ramos García huenda akatimiziwa anayoyahitaji kwenye klabu ya Real Madrid, kwa kupewa mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka mjini Madrid kwa miaka mingine ijayo.

Ramos amekuwa katika hali ya kukwaruzana na viongozi wake, kwa kuhitaji mkataba wenye heshima, hatua ambayo ilisababisha hofu baina ya mashabiki na wachezaji wengine klabuni hapo.

Raisi wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez amelazimika kusafiri hadi nchini China ambapo kikosi cha klabu hiyo kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya nchini Hispania, kwa lengo la kuzungumza na Ramos.

Perez atakutana na beki hyo hii leo na kufanya nae mazungumzo ya kina ili kumaliza mzozo uliokuwa unaendelea chini chini tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Man Utd, walikuwa wakihusishwa na mipango ya kutaka kumsajili Ramos, kwa kutumia mtego wa kumuhusisha mlinda mlango kutoka nchini Hispania, David de Gea nyumbani kwao Madrid kufuatia klabu y Real Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Kabla ya hapo Man Utd waliwasilisha ofa ya paund million 28 ambayo waliamini ilikua inatosha kumng’oa beki huyo mjini Madrid lakini uongozi wa klabu ya Real Madrid uliiweka kapuni ofa hiyo.

Man Utd, pia walijinasibu kuwa tayari kumlipa mshahara Ramos wa paund 200,000 kama kivutio cha kutaka ajiunge nao kwa msimu ujao

Mkataba wa sasa Ramos unafika kikomo baada ya miaka miwili.

Walichosema Dr. Slaa, J. Makamba, Peter Msigwa, Kuhusu Lowassa kuhamia Chadema
Sergio Romero Rasmi Man Utd