Rapa maarufu nchini wa Marekani, Caswell Senior maarufu Casanova amejisalimisha mikononi mwa Shirika la Kijasusi nchini Marekani (FBI) mara baada ya kutafutwa kwa siku kadhaa kutokana na agizo la kukamatwa kwake kwa tuhuma za kujihusisha na genge la kihalifu liitwalo, Untouchable Gorilla Stone Nation.

Shirika hilo lilitoa taarifa kupitia twitter, taarifa ambayo ilikuwa ikiueleza umma kuwa inawashikilia watu 17 wa genge hilo kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu, mauaji, dawa za kulevya na makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa ofisi ya mwanasheria Mkuu mjini New York, Casanova (34) pamoja na wenzake 17 wakikutwa na hatia basi watakutana na kifungo cha maisha gerezani.

Azerbaijan yatangaza idadi ya wanajeshi waliouwawa Karabakh
Sherehe za Uhuru zaahirishwa

Comments

comments