Rapa Azalea Banks amempa makavu Nicki Minaj kwa madai kuwa amekuwa akiogopa kuwakosoa wazungu pale wanapoleta ubaguzi wa rangi kwa wasanii wengine hadi pale inapomgusa yeye binafsi.

Nicki Minaj alilalamika hivi karibuni kuwa wasanii wa kike weusi wanapewa nafasi ndogo sana kwenye tuzo tofauti na mchango mkubwa waliouleta kwenye utamaduni wa pop. Malalamiko ya Nicki yanatokana kutoridhika na jinsi ambavyo hakupata nafasi kwenye kipengele cha Video Bora ya Mwaka katika tuzo za za video za MTV (MTV/VMAs).

Azalea ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi katika kiwanda cha muziki, amemkosoa Nicki wakati akijibu swali la shabiki wake katika mtandao wa kijamii aliyetaka kujua mtazamo wake kuhusu alichokisema rapa huyo wa Young Money.

“No because she only started speaking out when it affected her. And she always pulls a pu**y move and says … ‘that’s not what I meant’ trying to save with white audiences when she gets caught. (sic)” alitweet Azalea Banks.

Azalea Banks amekuwa katika mtafaruku na Nicki Minaj ambapo mwezi Mei mwaka huu wakati wa tuzo za BET, alimshambulia kwa maneno.

Magufuli Kufunga Barabara Za Dar Leo
Soldado Kurejeshwa Nchini Hispania