Mshambuliaji wa Simba, Raphael Kiongera yupo katika wakati mgumu ndani ya timu hiyo kwani tangu arejee akitokea KCB alikokuwa anacheza kwa mkopo hajafunga bao hata moja jambo ambalo limemfanya ashindwe kucheza kwa kujiamini.

Kiongera ambaye kwasasa ni majeruhi amesema kiwango anachokionyesha kwasasa kinamfanya awe mtu mwenye mawazo kwani haelewi ni kitu gani kinampata hadi ashindwe kufunga hata mabao mepesi.

“Bado naamini kuwa ipo siku nitafunga, huwa nashangaa siku hizi hata mazoezini sifanyi vizuri, sifungi kabisa wakati nikiona mpira najuwa kabisa kuwa naenda kufunga, yawezekana ni kwa vile nilicheza ligi muda mrefu halafu nikajiunga na Simba kwa kipindi kirefu ila nafasi ninazopata za kufunga ni rahisi.

“Kwa sasa siwezi kusema chochote zaidi namwachia Mungu na ninachokifanya sasa ni kusali sana na siwezi kusema labda ni mambo ya kishirikina kwani huwa siamini kabida hayo mambo,” alisema Kiongera

Kutokana na majeraha aliyonayo mshambuliaji huyo haelewi lini atarejea uwanjani kwani bado hajapatiwa matibabu wala vipimo vyovyote mpaka leo.

Florentino Perez Azima Ndoto Za Wapinzani
Membe azungumzia mpango wa kustaafu Siasa, aanza kuandika vitabu kama Sitta