Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anatarajia Beki kutoka nchini Ufaransa Raphael Varane kurejea katika utimamu wa mwili kwa wakati ili kushiriki katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA kati ya dhidi ya wapinzani wao wa jiji, Manchester City.
Varane alitolewa wakati wa mapumziko baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu wakati wa mchezo wa Mkondo wa Kwanza ya Robo Fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Sevilla, ambayo Mashetani Wekundu walipoteza kwa jumla ya mabao 5-2.
Beki mshirika wa kati wa Varane, Lisandro Martinez, alijeruhiwa kwenye mguu na hivyo hatakuwepo kwenye mchezo huo wa Fainali ambao utapigwa mwezi Juni.
Huku nahodha wa klabu hiyo Harry Maguire akiwa amesimamishwa, Luke Shaw alishirikiana na Victor Lindelof katikati ya safu ya ulinzi huku United ikifika fainali ya 21 ya Kombe la FA iliyoweka rekodi sawa na kwa ushindi wa mikwaju ya penalti Jumapili dhidi ya Brighton na Hove Albion.
United sasa itamenyana na wapinzani wao City wanaowinda kutwaa kwa mara ya mara tatu taji hilo katika fainali itakayopigwa Uwanja wa Wembley Juni 3, na Mashetani Wekundu wana matumaini ya kuwa na Varane.
Alipoulizwa kama Varane anaweza kushiriki fainali ya pili ya kombe la nyumbani la United msimu huu, Ten Hag aliiambia talkSPORT: “Nafikiri hivyo, ndio. Varane kwa fainali ya kombe hilo anaweza kurejea.” Varane ameichezea United jumla ya michezo 27.