Unaweza kusema Marcus Rashford  amefanikiwa kuibeba Manchester United Kwa kufunga  bao muhimu mbele ya timu ya Liverpool maarufu kama majogoo wa Anfield kwenye mchezo wa tisa wa Ligi kuu nchini uingereza.

Rashford alipachika bao hilo dakika ya 36 na kumuacha kwenye mataa mlinda mlango Allison na kuwafanya Liverpool waishiwe nguvu kipindi cha kwanza Uwanja wa Old Trafford.

Sadio Mane alipachika bao la kusawazisha dakika ya 43 teknolojia ya VAR ilikataa bao hilo kwa kuwa uligusa mkono kabla ya kuzama wavuni.

Video: Taifa satars wafunguka walivyopigwa mawe Sudan, Nchimbi awajibu wanaombeza

Iliwabidi Liverpool isubiri mpaka dakika ya 85 walipopachika bao lao la kusawazisha kupitia Adam Laliana na kuweka matokeo sawa.

Video: Mapya yaibuka!! Baraka Mpenja anafundishwa kutangaza na mwanamke, ‘chumbani napiga kelele’

Mchezo ulikuwa ni wa ubabe kwani kila mchezaji alikuwa kutokana na ugumu uliokuwepo uwanjani.

Liverpool imesalia kileleni ikiwa na alama 25 huku Manchester United ikiwa nafasi ya 10 na pointi zake 10.

Video: Kwa nini wanaume wagumu kuoa, Je tunahitaji upepo wa Kisulisuli? sababu zatajwa
'Boxer' tayari kuwavaa waarabu