Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford amemtaja mshambuliaji wa Mabingwa wa soka nchini England *Liverpool*, Sadio Mane kuwa ndiye mchezaji wa Kiafrika bora zaidi aliyewahi kukabiliana naye kwenye Ligi Kuu England.

Katika kipindi cha maswali na majibu cha Twitter, Rashford aliulizwa amtaje mchezaji bora zaidi wa Afrika aliyewahi kukabiliana naye kwenye ligi tangu alipoanza kucheza mwaka 2015.

Rashford alisema: “Nadhani kuna vipaji vingi vya Kiafrika kwenye ligi kwa wakati huu, mmoja wao ni Mane.”

Rashford amekabiliana na wachezaji mahiri kama Mohamed Salah, Yaya Toure, Pierre-Emerick Aubameyang na Riyad Mahrez, lakini anampa nafasi ya juu kabisa Mane.

Bocco, Mugalu wapewa kazi maalum Simba SC
Ibenge: Nipo tayari kwa matokeo yoyote