Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema wakati wa uongozi wake, atahakikisha anatumia rasimali zilizopo ndani ya Chama kutekeleza maslahi bora kwa watendaji wa chama, kuimarisha miundombinu, vitendea kazi, na vyombo vya usafiri.

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo hii leo Mei 6, 2023 katika mkutano wa viongozi wa CCM ngazi ya Shina, Majimbo, Wilaya, na Mkoa wakati wa ziara yake ya kuimarisha chama na kutembelea miradi mbalimbali, uliofanyika katika ukumbi wa Picadilly, Kombeni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, amewasihi viongozi wa ngazi zote wa Chama cha Mapinduzi kufuatilia na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ili kuhakikisha ahadi zilizotolewa zinatekelezwa katika maeneo yao.

Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa chama kinapaswa kuisimamia Serikali na kuzungumzia mambo mazuri yanayofanyika kwa wananchi. Utekelezaji wa miradi unaendelea, hivyo haiwezekani kwa chama tawala kushindwa kuongea kuhusu kufuatilia miradi ya maendeleo na utekelezaji wa ahadi zilizotolewa.

Tunachunguza kifo cha Nusura - Misime
Habari Picha: Sherehe kusikimwa ufalme, Charles wa III